WALIO NYONYA PAMOJA

Katika hadithi mtumi(rehma na amani ziwe juu yake) asema: “ni haramu kwa walio nyonyo pamoja yale ambao ni haramu kwa nasaba.”  Na katika hadithi nyengine asema kiasi cha mtu kuambiwa amenyonya na alie nyonya kwake awe kama mamake na watoto wake wawe kama ndugu zake kwa uharamu ni lazima mtu anyoyne mara tano kwa uchache akiwa mdogo.

Masomo yaliofanywa karibu yaonesha kuwa mtoto akinyonya kwa mwanamke zaidi ya mara tatu achukua baadhi ya sifa za kimaumbile (genetics) na hizi sifa za kimaumbile zinakua zafanana na ndugu yake alie nyonya nae, na imeonekana kua hizi sifa za kimaumbile zinao wakusanya watu walio nyonya pamoja lau wataowana yaweza kupelekea wapate maradhi, na hapa ndio yadhihir hikma ya dini na ilmu ya mtumi Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) kuharamisha watu walio nyonya pamoja kuowana.