KUNYWA MAJI KWA KUSMAMA

Katika hadithi ilopokewa na Anas na Qatada wasema mtumi(rehma na amani ziwe juu yake) amekataza mtu anywe maji kwa kusimama, wakamuuliza na kula jee? Akawambia hiyo ndio mbaya zaidi.
leo madaktari wasema mtu akila akiwa amekaa ni bora zaidi na ni salama kwake kwa sababu chakula na maji yateremka pole pole na vizuri tumboni, ama mtu akinywa maji kwa kusmama huwa yashuka kwanguvu tumboni na kugonga, na lau mtu ataendelea kula na kunywa kwa kusmama kwa mda itapelekea kuregea na kuteremka chini sehemu ya kusaga chakula na baadae kupelekea kuweko na uzito na kuchelewa kusagika kwa chakula.