MIUJIZA YA KULALA UBAVU WA KULIA

Katika hadithi mtumi (rehma na amani ziwe juu yake) asema: “ ukitaka kulala tawadhi kama unavo tawadhi kutaka kuswali kisha ulale kwa ubavu wako wa kulia….”

Baada ya qarne kumi na nne wasomi wamekuja kutwambia faida za kulala ubavu wa kulia, na katika faida za kulala ubavu wa kulia moyo haupati kulemewa na mapafu, kwani moyo uko upande wa kushoto sasa mtu akilali ubavu wake wa kushoto asababisha moyo ulemewe na mapafu kitendo ambacho chasababisha moyo kufanya kazi yake kwa shida, na ini liko upande wa kulia huwa lapata kutulia vuzuri pia ukilala kwa ubavu wako wa kulia chakula kilicho baki chasagika vizuri, na mtu akilala kwa tumbo apata tabu kutoa pumzi na pia viungo vyake vya siri huambatana na godoro ama kitanda kitu ambacho husababisha shah’wa na shah’wa husababisha kufanya ya haramu.