HAYAWANI MMOJA TU KATIKA MANII

Katika hadithi mtumi( rehma na amani ziwe juu yake) asema: “sio kwa maji yote(manii) ndio apatikana mtoto, na lau Mwenyezi Mungu ataka kujalia kuumba kitu basi hakuna kitu cha kuziwiya.”
hadithi hini mtumi (rehma na amani ziwe juu yake) aliulizwa na baadhi ya maswahaba zake kuhusu kupanga kizazi(family plan) ilkua mtu astarehe na mke wake akifikia kumaliza haja zake amaliza nje.

Katika qarne ya ishirini ndio wamekuja kungudua kuwa ni hayawani mmoja tu katika hayawani mia tatu milioni wanao toka katika manii ya mwanamume ndio anae penya akaingia kwenye kizazi cha mwanamke ndio kukapatikana mtoto kama Mwenyezi Mungu amejaalia kupatikane mtoto, maneno yaliosemwa na mtumi qarne kumi na nne “sio kwa maji yote(manii) ndio apatikana mtoto….”

Sasa kwanini hayawani mia mbili ama mia tatu milioni kasha mmoja tu ndi apenyeze kuingia katika kizazi cha mwanamke, na Mwenyezi Mungu asema katika Qur’an {hatukuumba mbingu na ardhi na ziliomo ndani yake bure….}??
jawabau ni kuwa hayawani mmoja peke yake haweza kupenyeza akafika kwenye kizazi cha mwanamke na kupasua aingie ndani, na kila hayawani katika manii ana mada kali ndio yasaidia kupasua kizuizi laini kilioko kwenye kizazi cha mwanamke ndio hayawani mmoja apate njia ya kupenyeza kwani, kisha hayawani wengi huwa wafa kabla ya kufika kufanya hio kazi ya kuchoma kizuizi kilioko kwenye kizazi cha mwanamke, na ndio pale utaskia madakatari wasema mtu huyu hawezi kuzaa kwa sababu manii yake ni kidogo, kwa sababu wakiwa kidogo inakua haiwezekani kufika kwenye kizazi cha mwanamke na kupasua.