KIZUIZI BEYNA YA BAHARI MBILI

(مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ * بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَا يَبْغِيَانِ)
(ameacha bahari mbili zikutane* beyna yake kuna kizuizi haziingiliani.)

Baada ya kuteremka aya hizi kwa qanre kumi na nne wasomi wamekuja kugundua na wamewahi kupiga picha wakiwa juu wakaona katika kila bahari kuna kizuizi cha kuzuia bahari zisiingiliane wala kuchanganyika maji yake na bahari nyengine bali kila bahari yabaki na sifa zake tofauti kama wingi wa chumvi na uzito wa maji yake na kila kitu chake chabaki vile vile, na wameona pia kua hicho kizuizi hakitulii bali chatembea kwa upepo na mfumo na kujaa kwa maji, hicho hicho kizuizi kiko katika maji ya bahari chumvi na maji matamu yam to, hayaingiliani maji ya chumvi nay a tamu wala samaki wa maji chumvi hawaingii kwenye maji tamu, asema Mwenyezi Mungu:

(وَهُوَ الَّذِي مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ هَذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ وَهَذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ وَجَعَلَ بَيْنَهُمَا بَرْزَخاً وَحِجْراً مَحْجُوراً)
(na yeye ndio ameacha bahri mbili zikutane, moja ni tamu sana na nyengine ni chumvi chungu, na akajali beina yake kizuizi na pingamizi ya kupinga zisiingiliane.)