MVUTO WA ARDHI

 

﴿اللَّهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا﴾
Mwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona

Kuna nguzo zimeziwiya mbingu lakini hamuzioni, baadhi ya wanazuoni wasema aya hii ni kama ishara ya kueleza kuhusu mvuto uliko katika kila sayari, kama mvuto ulioko kwenye ardhi unao vutia chini, na lau si hunu mvuto basi kungekuwa hakuna kitu kimetulia juu ya ardhi, katika aya nyengine:

(أَمَّنْ جَعَلَ الْأَرْضَ قَرَاراً)
(Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutulia)

Nani aliefanya kila kilioko juu ya aradhi kitulie? Hakika si kitu chengine ila ni huu mvuto alio uweke Mwenyezi Mungu, na lau mtu atatoka kwenye anga la ardhi basi atakua hana utulivu(balance) wala utulivu kama tunavo waona wale wanaotoka kwenda mwezini na sayari nyengine, na mwisho wa dunia itakosekana hunu mvuto na ardhi itatoa kila kiliomo ndani yake mpaka majabali yatapeperuka, Mwenyezi Mungu asema kwenye aya nyengine:

                                                      (وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ * وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ)                                                     
Na ardhi itakapo nyoshwa na kusawazishwa*Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tup)