FINGERPRINT

 

﴿أَيَحْسَبُ الْإِنْسَانُ أَلَّنْ نَجْمَعَ عِظَامَهُ * بَلَى قَادِرِينَ عَلَى أَنْ نُسَوِّيَ بَنَانَهُ﴾
Anadhani mwana adamu kuwa sisi hatutaikusanya mifupa yake? Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake

Yani mwanadamu anadhani kuwa mwenyezi Mungu hawezi kukusanya mifupa na kumrudisha tena hai siku ya kiama kwa hisabu ya siku hiyo.
aya hini yaonesha miujiza na utenda kazi wa mwenyezi Mungu katika kuumba mwili wa mwanadamu, wasomi wamegundua kuwa kila mwanadamu ana alama za vidole (fingerprint) tofauti na mwenzake hata kama ni pacha wamezaliwa kwa tone moja la manii, wala hakuna uwezekano wa wa kufanana (fingerprint) kivovote vile itakavo kuwa, na lau mwanadamu atakwatwa ngozi yake ya kidole basi ikimea itamea vile vile kama ilivyokua bila kubadilika alama na mistari ya (fingerprint) na ndio mwenyezi Mungu asema twaweza kukusanya mifupa yake tuiveshe na nyama na ngozi ya ncha ya vidole vyake irudi kama ilivyokua pia.