HADITHI YA ARUBAINI NA MBILI-MSAMAH WA MUNGU

[عن أنس رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم يَقُولُ: " قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي. يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ . يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لاَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً."] رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.

[ kutoka kwa Anas (Mungu awe radhi nae) asema: nilimsikia mtumi wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani ziwe juu yake) akisema: “ asema Mwenyezi Mungu alie tukuka: ewe mwana adamu, hakika wewe huniombi mimi ukitarajia nikusamehe ela nitakusamehe wala sijali, ewe mwana adamu, lau madhambi yako yatakua makubwa kufikia mawingu kisha ukaniomba msamaha nitakusamehe, ewe mwana adamu, lau utanijia na madhambi mengi kiasi cha ukubwa wa ardhi kisha ukanikuta mimi ukiwa hujanishirikisha na kitu chochote nitakujia na msamaha kama madhambi yako.”] imepokewa na Imam Tirmidhy.