HADITHI YA ARUBAINI-MPITA NJIA

[عن ابنِ عُمَرَ رضي اللهُ عنهما قال: أَخَذَ رسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم بِمَنْكِبيَّ فقال:"كُنْ في الدُّنْيا كأنَّكَ غَرِيبٌ، أو عابرُ سبِيلٍ."
وكانَ ابنُ عُمَرَ رَضي اللهُ عنهما يقولُ: إذا أمْسَيْتَ فلا تَنْتظِرِ الصبَّاحَ، وإذا أصْبَحْتَ فلا تَنْتَظِرِ الَمسَاءَ، وخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرضِكَ، ومِنْ حَياتِكَ لِمَوْتِكَ.] رَوَاهُ الْبُخَارِي.

[kutoka kwa Ibnu Umar (Mungu awe radhi nae) amesema: mtumi (rehma na amani ziwe juu yake) alinishika bega  akaniambia: “ kuwa katika dunia kama mgeni ama mpita njia.”
na Ibnu Umar (Mungu awe radhi nae) alikua akisema: ukiingiliwa na jioni usisubiri asbuhi, na ukipambaukiwa usisubiri jioni, na patiliza afya yako (kufanya mazuri)  kabla hujashikwa na ugonjwa, patiliza uhai wako kabla hujafa.] imepokewa na Imam Bukhary.