HADITHI YA THALATHINI NA NNE-KATAZA MABAYA

[عن أبي سعيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقوُل: " مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَراً فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإنْ لمَ يَسْتَطِعْ فَبلِسانِهِ، فَإنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أضْعَفُ اْلإِيمَانِ."] رَوَاهُ مُسْلِمٌ

[kutoka kwa Abu Saed Alkhudhry (Mungu awe radhi nae) asema: nilimsikia mtumi wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani ziwe juu yake) akisema: “ mwenye kuona mabaya akomeshe  kwa mkono wake, kama hawezi,akanye kwa ulimi wake, kama hawezi,achukie kwa moyo wake na huko (kuchukia tu kwa moyo) ndio daraja dhaifu ya imani.” ] imepokewa na Imam Muslim.