Ni nini Miujiza ya Qur'an?

بسم الله الرحمن الرحيم

(سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنْفُسِهِمْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ. 41:53)
Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie wazi kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ndie Shahidi wa kila kitu.

Ni nini Miujiza?
Miujiza ni kitu ambacho mwanadamu hawezi kufanya kawaida ila kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kama walivopewa miujiza mitumi waliotangulia,moto kutomchoma Ibrahim,kusema udogoni na kuhuisha maiti kwa nabii Isaa,kupasua bahari kwa fimbo ya nabii Musa na miujiza ya mtumi Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) ni Qur’an ni ndio Miujiza mikubwa ambayo mpaka leo wasomi waendelea kuona miujiza na ilmu mbali mbali zilioko ndani ya Qur’an, na kila mtumi alie pewa miujiza ilkua ni miujiza ya kushindana na uhodari wa kufanya jambo ambao watu wake walokua wajulikana wao ndio mahodari zaidi kwa wakati wao kama nabii Musa wakati wake ilkua ni uchawi ndio akapewa fimbo iliokua ikibadilika kuwa nyoka mkubwa kiasi wachawi waliokua wajua kazi yao walikua waelewa kuwa huu aliokuja nao Musa sio uchawi bali ni miujiza ya kutoka kwa Mwenyezi Mungu na wakaamini waliona ukweli, na  Mtumi Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) alipotumilizwa na kupewa amri ya kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu ilkua waarabu wako kiwango cha juu kabisa katika lugha yao kwa dalili ya tungo zao za wakati huo, ikateremshwa Qur’an wakaamini walio amini na kukubali kuwa lugha ya Qur’an ilivyopangakika na ilivyo faswaha zaidi haiwezikani kuwa mtumi ameitunga yeye kama walivyokua wakidai waliokuwa wakipinga huku wengine wakisema ni uchawi na maneno mengi ya kupinga na huku Qur’an ikijitetea na kurudi hoja zao zisokua na msingi…. (au wanasema ameizua? Wambie: leteni sura kumi zilizo zuliwa mfano wa Qur’an na muiteni munae mtaka awasaidie kuzusha asie kua Mwenyezi Mungu mukiwa  ni wakweli, wasipo weza basi jueni kuwa hii Qur’an imeteremshwa kwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu na mujue kuwa hakuna Mungu anae faa kuabudiwa kwa haki ila yeye basi hamuslimu? 11:14-15) na katika aya nyengine (na ikiwa muna shaka na tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja tu mfano wa Qur’an na muite mashahidi wenu wasio kua Mwenyezi Mungu mukiwa ni wakweli, na ikiwa hamuwezi na wala hamutowez basi ogopeni moto….. 2:23-24)

Miujiza ya mitume waliotangulia ilimalizika kwa kufa wao lakini miujiza ya Qur’an bado yaendelea mpaka leo, kwani mpaka leo hakuna alie weza kuleta tungo kama ya Qur’an wala hakuna atakae kuweza kutunga kama Qur’an kwa ushahidi wa Qur’an

Na miujiza ya mtumi Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) haikuwa Qur’an peke yake bali kuna miujiza mengi ambayo imeelzwa kwa upana na walio andika tarekhe na sera ya bwana Mtumi (rehma na amani ziwe juu yake) kama kupasuka kwa mwezi, kutoka maji katika kitanga chake cha mkono kitukufu, kufinikwa kwa kivuli cha mawingo anapo tembea, kumuona alioko nyuma yake kama alioko mbele yake, na mengine mengi ambao hapa sio mahali pake bali hapa tumekusudia kueleza miujiza ya Qur’an peke yake ambayo bado yaendelea mpaka mwisho wa dunia…. Wa billahi tawfeeq.