HADITHI YA KWANZA-NIA

بسم الله الرحمن الحيم

{عن أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: "إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى، فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا يُصِيبُها أو امْرأةٍ يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه"} رواه البخاري ومسلم.

{Kutoka kwa Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattaab (Mungu awe radhi nae) asema : Nilimsikia mtumi wa Mwenyezi  Mungu (rehma na amaani ziwe juu yake) akisema: Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokusudia.  Kwa hivyo mwenye kugura  kwa ajili ya Allaah na Mtumi wake, kugura kwake ni kwa ajili ya Allaah na Mtumi wake, na  yule ambae  amegura kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (Fulani) basi kugura kwake itakua ni kwa hicho alicho kiendea.} Imepokewa na Imam Bukhary na Muslim.