HADITHI YA NNE-QADAR NA MWISHO WA MWANADAMU

 

 عن أبي عبْدِ الرَّحْمن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قال: حدَّثَنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وهُوَ الصَّادقُ المَصْدوق: " إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يُرْسَلُ إليه المَلكُ فَيَنْفخُ فيه الرُّوحَ ويُؤمَرُ بأرْبَعِ كلماتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ وأَجَلِهِ وعَمَلِهِ وشَقيٌّ أو سَعيدٌ، فَوَاللهِ الَّذي لا إله غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ ليَعْمَلُ بعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ حتى ما يكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَليْه الكِتابُ فَيَعْمَلُ بعَملِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُها. وإنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهل النَّارِ حتى ما يَكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكتابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهل الجنَّةِ فَيَدْخُلُها " ] رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ

[ Kutoka kwa Abu Abdulahman  Abdullaah Ibn Masu'ud (mungu awe radhi nae) asema: alitueleza haya mtumi (rehma na amani ziwe juu yake) naye ndie mkweli, anaesadikiwa: “ Hakika umbo la kila mmoja wenu linakusanywa  pamoja katika tumbo la mama yake kwa muda wa siku arubaini, ikiwa katika hali ya tone la manii, baadaye tone la damu kwa muda kama huo, kisha huwa ni kipande cha nyama kwa muda kama huo, kisha hupelekwa  Malaika kumtia ruhu na anaamrishwa mambo manne:  kuandika rizki yake, maisha yake, amali yake na akiwa atakuwa (mtu) mbaya au mwema, naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna Mungu isipokuwa Yeye, mmoja katika nyinyi hufanya vitendo vya watu wa peponi mpaka iwe hakuna baina yake na pepo ila mfano wa dhiraa moja tu kikatangulia kilichoandikwa akafanya amali ya watu wa motoni akaingia motoni,  na mmoja katika nyinyi hufanya amali  ya watu wa motoni mpaka ikawa hakuna baina yake  na moto ila mfano wa dhiraa moja tu,kikatangulia kilichoandikwa akafanya amali ya watu wa peponi akaingia peponi.] Imepokewa na Imam Bukhary.