Waliokua haramu kuwaowa kwa kunyonya

BISMILLAAH


ALMUHARRAMAAT 2:

 Baada ya kutaja wanawake ambao ni haramu kuwaoa kutokana na nasaba nao ni wasaba, sasa tutataja saba wengine ambao ni haramu kuwaoa kutokamana na kunyonya, kisha tutamalizia wanne amabao ni kutokamana na ukwe, tukiwa tunamaliza kuwataja fungu lakwanza ambao ni haramu milele kuwaoa.

Anasema Mtume s.a.w katika hadithi iliyopokewa na Imam Bukhary: wanaokua haramu kwa nasaba hua haramu pia kwa kunyonya.

kwakua kwa nasaba walikua ni wasaba, na pia kwa kunyonya ni saba, nao ni kama wafuatavyo:

1: Mama kwa kunyonya. 
 Nae ni kila mwanamke aliyekunyonyesha ama aliyemnyonyesha aliyekunyonyesha wewe ama yule uliyekunywa maziwa yake hata kama si kwa njia ya kunyonya. Pia aliyemnyonyesha babako, na mama ya  aliyekunyonyesha, na mama wa mwenye maziwa.
NB: Mwenye maziwa ni mume wa mwanamke aliyekunyonyesha.

2: Binti kwa kunyonya. 
 Nae ni kila binti alienyonyeshwa maziwa yako, ama alienyonya kwa binti yako, ama alienyonya kwa mwanamke uliemzalisha, na banati zao kwa nasaba na kunyonya pia.

3:Dada kwa kunyonya. 
 Nae ni kila aliyenyonyeshwa na mamako, ama aliyenyonyeshwa maziwa ya babako, ama binti ya aliyekunyonyesha wewe, ama aliezaliwa na mwanamume uliekunywa maziwa yake.

4: Shangazi kwa kunyonya.
 Nae ni kila dada wa mwanamume ulienyonya maziwa yake, ama shangazi ya uliekunywa maziwa yake.

5: Khale kwa kunyonya. 
 Nae ni kila dada wa aliyekunyonyesha, ama khale yake aliyekunyonyesha, sawa kwa nasaba ama kunyonya.

6,7: Binti wa kaka na bint wa dada kwa kunyonya. 
 kila binti aliezaliwa na watoto wa aliyekunyonyesha ama mwenye maziwa, sawa kwa kunyonya ama kwa nasaba. Na pia kila mwanamke aliyenyonyeshwa na dadako, ama alienyonya maziwa ya kakako, na banati zake, na banati wa watoto wake, sawa kwa nasaba ama kwa kunyonya. 

 

Wallaahu a'lam.