Waliokua haramu kuwaowa kwa nasaba

BISMILLAAH

ALMUHARRAMAAT   1

 Wanawake ambao ni haramu kwa mwanamume kuwaoa ni kila ambaekwamba ni haramu kumuoa kwa nasaba, kunyonya na ukwe, na wako sampuli mbili:

1: Wanaokua haramu kwake milele.

2: Wanaokua haramu kwake katika kuwajumuisha.

Tukianza na fungu la kwanza, nao wapo kumi na nane, wasaba kwa nasaba, nao wametajwa katika Qur'an, nao ni kama wafatao:

1: Mama. Nae ni kila mwanamke ambae nasaba yako inaisha kwake, sawa kwa kupitia kwa mwanamume ama mwanamke. Anaingia mama wa kukuzaa na bibi yako upande wa baba na pia upande wa mama, na mama zao....na kuendelea hivyo.

N.B: wako mama ambao ni haramu kwetu kuwaoa lakini haziishi kwao nasaba zetu, nao ni wake za Mtume s.a.w ambao ni mama wa waumini.

2: Binti. Nae ni kila mwanamke ambae nasaba yake inaisha kwako. Nao ni binti yako na binti wa mwanao wakiume, na binti wa mwanao wakike....na kuendelea hivo.

3: Dada. Nae ni kila mwanamke aliezaliwa na wazazi wako wawili ama mmoja wao.

4: Shangazi. Nae ni kila mwanamke ambae ni dada ya mwanamume aliekuzaa, sawa ikiwa ni dada wa hakika kama shangazi, ama dada wa majazi kama shangazi yake baba, na anaweza kua upande wa mama kama dadake babu upande wa mama.

5: Khale. Nae ni kila mwanamke ambae ni dada ya mwanamke aliekuzaa, sawa ikiwa ni wa hakika kama khale, ama wa majazi kama khale yake mama.

6: Binti wa kaka, na banati zao, na banati wa banati zao..... namna itakavyoshuka.

7: Binti wa dada, na banati zao, na banati wa banati zao..... namna itakavyoshuka.

 

 Wallaahu a'lam.