KISWA CHA ISRA NA MIRAJ

 

 

 

(سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ

إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ

آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ)

(Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Aqswa, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.)

Mtumi alpozodiwa na dhiki za kidunia kwa kufiliwa na mkewake msaidizi wake nana Khadija na Ammi yake Abutwalib aliekua ngao yake aliekua akimkinga na maudhi ya maqureyshi wa Makkah na baada yakuenda mji wa Twaif kutaka kuwalingania watu uislamu na kuoneshwa idhalali ya kupigwa kwa mawe mpaka mwili wake mtukufu ukienea damu, hapo ndio Mwenyezi mungu alimpangia safari ya kumpambaza na haya maudhiko ya kidunia na kumpunguzia huzuni aliokuwa nazo, Mwenyezi mungu alimsafirisha Mtumi wake katika usiku mmoja kutoka mji wa Makkah hadi msikiti wa Aqswa ulioko Falastina na kumpaza kitoka msikiti wa Aqsa mpaka mbingu ya saba kwenda kuonana na Mola wake.

Hakika wanazuoni wametofautiana katika tukio la Isaraa na Miraj, je Mtumi alikwenda safari hii kwa kiwiliwili chake kitukufu akiwa macho ama safari hii ilkua ya ndotoni na ingawa ndoto za mitumi huwa ni mambo ya hakika lakini qauli yeneye nguvu ni kuwa Mtumi (rehma na amani ziwe juu yake) alikwenda kwa kiwiliwili chake kitukufu akiwa macho na afahamu kila kitu, na tukio hili lilikua  kabla ya Mtumi  ( rehma na amani ziwe juu yake) kugura kutoka Makkah kuenda Madina.

Kiswa cha Isaraa na Miraj kama anavo tuelezea Albarazanjy chaanzia Mtumi  (rehma na amani ziwe juu yake) alpokua amelala karibu na maqam Ibrahim wakaja malaika Jibril na Mikail wakampasua kifua chake wakatoa moyo wake mtukufu wakausafisha kwa maji ya zamzam wakanjaza imani na ilimu na hikma kisha wakampiga muhuri wa utumi beyna ya mavega yake, kisha akaletewa Buraq akiwa amepambwa na anaesifika kwa kila sifa za hayawani mwenye kwenda mbio sana, wakaanza safari malaika Jibril na Mikail wakiwa kulia na kushoto, wakapita kwenye ardhi yenye mitende yenye mitende mizuri Jibril akamwambia hapa ndio Twaybah(Madina) na hapa ndio utagura na utakufa, kisha wakapita mahali Jibril akamwambia swali hapa hapa ndio kuna mti ule wa fimbo ya nabii Musa fimbo iliopasua bahari, wakienda mbele akamwambia shuka tena hapa uswali hapa ndio jabali Sinai, jabali lile nabii Musa alizungumza na Mola wake, kisha wakapita sehemu kuna majumba makubwa Jibril akamwambia swali hapa, hapa ndio Bethlehem alipozaliwa nabii Isa, katika safari yao walipambana na jini alikua amebeba  moto, kila mtumi akizunguka amuona awafuata hapo jibril akamfundisha dua akasoma akapotea yule jini, katika safari yao waliona watu walima wakivuna kwa mda wa siku mbili, Mtumi akamuuliza Jibril ni nani hawa Jibril akamjibu hawa ni watu wanaopigana jihad wanavolipwa mema yao, kisha Mtumi akaskia harufu mzuri na akamuona yule aliekua akimsonga nyele mtoto wa Firauni alpoangukiwa na kishanua akasema "bismillah ameangamia Firauni hakika amepotea" binti ya Firauni alvoskia hivo akauliza " Kwani wewe una Mola mwengine asiekua babangu?" Akajibiwa naam Mola wangu na Mola wako ni yule alie muumba babako Firauni alipopata khabari hii akamchoma yeye na mumewe na watoto wao, Mtumi (rehma na amani ziwe juu yake) alipita akaona watu wakatwa vitwa zikirudi kumea kama zilvokuwa, akauliza ni watu gani hawa? Akaambiwa hawa ni watu wanaofanya uvivu kuswali, kisha akapita sehemu nyengine akaona watu nguo zao zimejaa viraka mbele na nyuma huku wameuma meno mti wa zaqqum, mti wa  motoni, akauliza na hawa ni kina nani? Akaambiwa hawa ni watu waliokuwa hawatoi zaka za mali na haya ndio malipo yao wala hawakudhulumiwa, kisha akaona watu wala nyama mbichi na karibu kunao nyama ambayo imeiva vizuri sana, akaambiwa hawa ni watu wameowa/wameolewa kisha watafuta zina nje, hawa ni wazinifu, kisha akona mbao katikati ya njia kila kinachopita karibu chakatika, akaambiwa huu ni mfano wa watu katika umati wako wanaovamia wenzao mali yao wakiwa safarini, kuendelea na safari akaona mtu amebeba mzigo mkubwa asiouweza na hataki kupunguza bali ataka kuongeza, akaambiwa huyu ni mtu huwa na amana nyingi za watu na akashindwa kutekeleza amana za wenyewe na bado aendelea kupokea amana, akaona wengine ndimi zao zavutwa kwa chuma kila zikikatika zarudi kumea tena zikikatika, akaambiwa hawa ni  makhatibu katika umati wako watoa mawaedha waambia watu maneno mazuri wasiyoyatenda, kisha akaona watu wengine wajikata nyuso zao na vifua vyao kwa kucha za shaba, akauliza ni nani hawa? Akaambiwa hawa ni watu wakusengenya na kuvunia watu heshima zao, kisha akaona ng'ombe atoka kwenye tundu kisha ajaribu kurudi na hawezi, akaambiwa huu ni mfano wa mtu husema maovu akajutia lakini hawezi kujitetea, kiendelea na safari wakapita kwenye uwanja wenye harufu na sauti mzuri, sauti yasema " ewe Mola nipe ulichoniahidi hakika uwanja wangu umejaa mazuri yasomfano" akaambiwa ni sauti ya pepo ilioandaliwa wanaume na wanawake wenye jutenda mema, kasha akapita kwenye uwanja mwengine wenye harufu na sauti mbaya wasema " ewe Mola nipe ulichoniahidi hakika uwanja wangu umejaa adhabu ambazo wenye madhambi hawawezi kuvumilia" akaambiwa hii ni sauti ya moto wa jahannam, kuendelea na safari akaona malaika wamebeba kitu chenye mwangaza mwingi sana kushinda nyota za kung'ara, akiwauliza wakamwambia ni nuru ya uislamu tumeamrishwa tuweke sehemu za Sham, katika kutembea Mtumi  (rehma na amani ziwe juu yake) akalinganiwa na myahudi upande wa kulia, Jibril akamwambia lau ungemjibu basi umati wako wote wangekuwa mayahudi, na upande wa kushotoakalinganiwa na mnaswara, akaambiwa lau ungemjibu basi umati wako wangekua manaswara, akakutana na mwanamke alikua amejirembesha kwa kila aina ya mapambo akamuita  Mtumi akampuuza, jibril akamwambia huyu mwanamke ni mfano wa dunia na lau ungemuitikia basi umati wako wangependa dunia zaidj na kudharau akhera, baada yake Mtumi  (rehma na amani ziwe juu yake) aliona mzee mkongwe uko kando ya barabara huku akimuita, Jibril akamwambia usimsikize huyu ndie adui aliyemtoa Adam peponi, huyu ataka umkurubie ufuate upotevu, huyu ni shetani alie laaniwa, kisha Mtumi  (rehma na amani ziwe juu yake) alipita akaona kinyanya kikongwe kando ya barabara akmuita Mtumi akampuuza, Jibril akamwambia ulimwengu siku zake zimebaki chache sana kama umri wa huyu mkongwe, kisha Mtumi akakutana na watu nyuso zao zang'ara kama taa wakamsalimia Mtumi  ( rehma na amani ziwe juu yake) akawajibu salamu, Jibril akamwambia hawa ni manabii, Ibrahim, Musa na Isa, kisha akampotia nabii Musa akiwa aswali kwenye qabri yake akapanda kumsalimia Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yao) kisha nabii Musa akauliza huyu ni nani? Jibril akamwambia huyu ni Muhammad, nabii Musa akmkurubisha na kumwambia waombee umati wako wepesi na salama, kisha Mtumi akaulizia huyu ni nani nabii akamjibu mimi ni Musa mtumi wa wana wa Israeli, kisha Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake) akapita kwenye mti chini yake kulkua kumekaa mzee na watoto wake akaona na nuru imewaenea, akaambiwa huyu ni babako Ibrahim, akamsalimia na nabii Ibrahim akampokea vizuri na kumsifu alpoambiwa huyu ni mtoto wako Ahmad aliebashiriwa katika vitabu, akaendelea na safari yake akapita mji wa Maqdisiyyah akona Jahannam na moto unavoruka ukubwa wake kama majumba makubwa hutishika mwenye kuuona, akaingia mjini kwa upande wa kulia akaenda kuona msikiti wenye nuru upande wa kulia na kushoto akauliza hizi nuru gani? Jibril akamwambia upande wa kushoto ni qabri ya nana Maryam na kulia ni sehemu aliokuwa akiswali nabii Daud, wakaingia msikitini kuswali hapo hapo kukaadhiniwa na watu wakakusanyika na  Mtumi  ( rehma na amani ziwe juu yake) akatangulia kuwasalisha, kisha mtu akakutana na roho za manabii (rehma na amani ziwe juu yao) wakamsifu kwa kila kwa sifa alizopewa na Mola wake na Mtumi akamshukuru Mola wake kumtumiliza akiwa ni rahma kwa walimwengu wote na kufanya ummah wake ndio ummah wa kati na wa mwisho kuumbwa na ndio wakwanza kuingia peponi, akaendelea kumshukuru Mola wake kwa kukuza jina lake, manabij wakaanza kuzungumza na mtumi huku wakiulizana mambo ya qiyama na dalili zake na nabii Isa akataja baadhi ya dalili za qiyama na Mtumi akachangia kwa kusema kuwa hakika mimi nimetumilizwa na qiyama kimekurubia kama zilokurubiana vodole vyangu vya kati, kisha Mtumi  ( rehma na amani ziwe juu yake) akashikwa na kiu akaletewa maziwa na asali na maji na khamri, akanya asali mwanzo kisha akamaliza kwa maziwa mpaka akamaliza kiu yake, Jibril akamwambia umefanya kama inavotaka dini, na lau ungekunywa khamri basi umati wako wangalia potea sana na kama ungekunywa maji umati wako wangegharikishwa kwa maji.

Baada ya hii safari ndefu ya duniani Mtumi  ( rehma na amani ziwe juu yake) alifika kwenye ngazi ile inayopandishiw roho za watu wanapokufa, ngazi  mzuri isio kifani, wakapanda yeye na Jibril mpaka wakafika kwenye mlango wa mbingu ya kwanza, Jibril akaomba kufunguliwa wakafungilwa, katika mbingu ya kwanza wakakutana na Adam wakasalimiana kisha akapanda mbingu ya pili akakutana na nabii Isa na Yahya, wakasilimiana wakaombeana kisha akapanda mbingu ya tatu akakutana na nabii Yusuf yule aliepewa nusu wa uzuri wa Mtumi  ( rehma na amani ziwe juu yao) wakasilimiana kisha akapanda mbingu ya nne wakifunguliwa mlango wakakitana na nabii Idris wakasilimiana na kuombeana mazuri wakaagana Mtumi akapanda mbingu ya tano, kwenye mbingu ya tano alikutana nabii Harun, akapamda mbingu ya sita akakutana na musa akiwa na wafuasi wengi walokua wamemuamini, kisha nabii Musa akamwambia enua uso wako uangalie umati wako wao ni wengi zaidi na wao ndio wataingia peponi wengi zaidi, kisha Mtumi akapanda mbingu ya saba akaskia radi na pepe akaskia na malaika wamsabihi Mola wao, kisha akakutana na nabii Ibrahim katika mlango wa pepo, nabii Ibrahim akamwambia wahimize umati wako wakithirishe makulima ya peponi na hakika makulima ya peponi ni kusema "la haula wala quwata illa billah" Kisha akaona watu wamekaa na nabii Ibrahim, wengine nyuso zao zang'ara na wengine nyuso zao bado zina weusi, wale walokua na weuso nyuso zao wakaamka na kuingia kwenye mto wakatoka wakiwa wang'ara nyuso zao, akauliza ni hawa ni watu gani na huu mto ni vp? Ndio akaambiwa hawa watu wenye nyuso za kung'ara ni watu wafanya ibada na kumtwii Mola wao, na hawa walokua na weusi wa uso ni watu wafanya madhambi na ibada, huu mto mdio mfanya wa rehma za Mwenyezi mungu na hapa ni peponi, kisha Mtumi  ( rehmana amani ziwe juu yake) akapandishwa sidratul muntaha mahali zinapopelekwa roho za waumini peponi na akaambiwa kuwa haya ndio mashukiza ya waliokuamini katika umati zako ndani kuna kila aina ya starehe na mapambo, kisha akaingia peponi, pepo ambayo haijawahi kuonekana wala hakuna mtu ameweza kufkiria starehe zilioko ndani yake, akaona kuwa mema hulipwa mara kumi na mwenye kukopesha wenzake hulipwa mara kumi na nane, akauliza ni vp mambo haya? Akaambiwa kuwa mtu kutoa chake kumkopesha mwenzake si jambo rahisi ndio maana malipo yake yakawa makubwa, kisha akamuona hurulaini wa Zaid bin Harithah (swahaba) akaona mchanga wa pepo ni miski, kisha akaskia sauti ya mtu atembea kwenye pepo akaambiwa hoyo ni Bilal (swahaba), kiendelea na safari yake kuelekea kumuona Mola wake akaoneshwa moto mwenye sura ya utisho kwa makafiri, kisha mtumi akapanda zaidi mpaka akaskia sauti ya kalamu inayo andika qadar za waja, akaona mtu amezama kwenye nuru ya arshi, akauliza ni nani huyu? Ni malika ama ni mtu? Akaambiwa huyu ni mtu katika umati wako ulimi wake ulikoa haukauki kwa kumtaja mola wake (dhikri) na moyo wake ulikua umefungamana sana na misikiti ndio akafika hapa alipofika, akaenda Mtumi  ( rehmana amani ziwe juu yake) mpaka akamkurubia mola wake, hapa ndipo Jibril alismama na akamwambia hapa ulipofika sasa mimi siwezi tena kusonga mbele, na nitasonga mbele zaidi ya hapa basi nitadeuka na nitapotea kabisa kwa nuru ya dhati ya Mwenyezi Mungu,  hakika kila mtu ana mipaka yake hafai kupita, Mtumi ( rehmana amani ziwe juu yake) akaendelea na safari yake peke yake hapo ndio Mola wake akataka kumpumbaza zaidi akamletea malaika kwa sura za rafiki wa katibu zaidi Abubakar Swidiq akimpumbaza njiani mapaka akafika kwa Mola wake na akapomoka kusijudu, Mtumi  ( rehmana amani ziwe juu yake ) akamuona Mola wake kwa macho yake, kisha akaambiwa aombe anachotaka na atapewa, akamwambia Mola wake hakika wewe umemfanya Ibrahim rafiki yake na Musa umezungumza nae, na Isa umemfundisha Injil na Taurati na ukamlinde yeye na mamake, Mwenyezi mungu akamwambia na wewe nimekufanya kipenzi changu wa karibu sana na  nimekupa Qur'an na uislamu, na nimekupa swala khamsini muzismamishe wewe na umati wako, hizi ndio zawadi alopewa Mtumi katika safari yake hii tukufu, wakati wa kushuka na kurudi zake duniani akapita akamuona nabii Musa akamuuliza amekupa nini Mola wako? Akamwambia nimepewa swala khamsini niziswali na umati wangu asbuhi na jioni, nabii Musa akamwambia rudi kwa mola wako na umwambie akufanyie sahali manake umati wako ni dhaifu hawatoweza kutekeleza hii ibada ya swala khamsini kwa siku, akarudi kwa mola wake akaomba kufanyiwa sahali mara mbili mapaka zikafika tano  nazo ni hizi tunazo ziswali sasa, na akaambiwa kuwa hizi tano moja thawabu yake ni kama kumi kwahvo ni swala tano lakini malipo yake ni khamsini, na mema hulipwa mara kumi kwa moja, na mwenye kuwa na nia ya kufanya mema na asiweze kufanya pia ataandikiwa thawabu, na baya lalipwa kwa mfano wake, na mwenye kutaka kufanya baya kisha asifanye haandikiwi madhambi yoyote.

Mtumi alpokua ashuka sasa kila anapopita alikua akiusiwa awambie umayi wake wakithirishe kuumika(kufanya hijama)Alpofika mbingu ya kwanza akona moshi na sauti kubwa, akamuuliza Jibril, Jibril akamwambia hawa na mashetani wawapinga binadamu kuangalia juu ni kufikiria utendakzi wa mungu.

Alipofika ardhini akapanda kuelekea alipotokea (Makkah) akapambana na msafara wa maqureysh na alipokurubia kuna ngamia aligutu na akaumia mguu, akapambana na masafara mwengine walikua wamepoteza ngamia wao, Mtumi akawasalimia na baadhi yao wakatumbua sauti ya Mtumi lakini kwa shaka, akafika Makkah kabla ya asbuhi ya usiku ule ule alionda hyo safari ya Israa na Miraj,  kulipo pambuzuka Mtumi alikua na huzuni akifkiria kuwa lau ataelezea watu hii safari yake basi watu watamuona mrongo haswa wale makafiri wa kiqureysh, na kama alvokua akikhofia Abu jahli alimpitia na kumuuliza jee kuna khabari umetuletea ewe Muhammad? Huku akimfanyia stihzai na kumuudhi, na bila ya khofu yoyote ya kujiamini na ukweli wake Mtumi alimwambia ndio nimekuja na khabari mpya, hakika jana usiku nilipelekwa safari ya kwenda Qudsi (Falastina), Abu jahla akamuuliza kwa stihzai "kisha umerudi Makkah leo leo?!" Akamjibu ndio, Abujahli akamuuliza jee nikikuitia jamaa zako wote utawambia kuhusu safari yako kama ulivyo niambia mimi? Mtumi akamwambia ndio, wakaitwa watu Mtumi akawaelezea kwa ushujaa kamili, walomuamini wakumuamini na wengine wakawa wamfanyia shere na stihzai huku wakimwambia hakika sisi twaenda Falastina kwa muda wa miezi miwili kisha ww leo waja kutwambia umeenda kwa usiku mmoja na ukarudi usiku huo huo!! Abubakar Swidiq akamtetea akiwambia maqureysh hakika mimi namuamini Muhammad na kila atakalo kulisema ni kweli, maqureysh wakataka Mtumi awasifie msikiti wa Qudsi ulivyo na hapo Mtumi akaanza kuwasifia vile alivyo uona, wakamuuliza kitu kimoja kimoja katika vitu vya msikiti wa Qudsi na akawa awaelezea kama kwamba auona mbele yake huku Abubakar Swidiq akisema umesema ukweli na mimi naamini kuwa wewe ni Mtumi wa mwenyezi mungu mapaka maqureysh wakaamini kuwa hizi sifa za msikiti zinavo elezwa ni kuwa Mtumi ameona kweli huu msikiti na amepata alivyo usifu, wakamuuliza pia kuhusu ile misafara alioiona akawasifia kama alivyo iona na akawambia watafika Makkah siku kadhaa na sjku hiyo hiyo.

Mpaka hapa ndio mwisho wa kiswa hichi cha Isaraa na Miraj, kiswa hichi kina mazingatiwa mengi ndani yake na mafundisho mengi ambayo utayapata sehemu nyengine inshallah.