FATIMAH AZZAHRAA

Kwa mnasaba wa kuzaliwa nana wa wanawake wote wa ulimwenguni Fatma bint rasulillah twawaletea historia yake kwa ufupi. Yeye ni Fatma binti ya mtumi wa mwenyezi mungu, alizaliwa katika mji wa Makkah katika tarehe ishirini ya mfungo tisa kabla ya miaka mitano ya kutumilizwa kwa bwana mtumi rehma na amani ziwe juu yake, nana Fatma ndie binti ya mtumi wa mwisho na ndie alkua apendekeza zaidi mbele ya babake na pia kizazi cha mtumi chote kimepitia kwa nana Fatma. Mama yake ni nana Kahadija yule alie simama na mtumi kwa hali na mali kuinusuru dini. Kuzaliwa kwake: Ilipo kurubia kuzaliwa kwake mtumi alimwambia nana Kadijaa, ewe Khadija! Jibril amekuja kunipa bishara kuwa mimba yako ni ya mtoto wa kike na ndie pumzi iliotwahara na baraka, na mwenyezi mungu atajalia kizazi changu kupitia kwake na katika kizazi chake kutatazaliwa viongozi ambao watakua makhalifa katika ardhi yake. Majina yake: Nana Fatma alikua na majina tisa mashhuri zaidi: Fatma.. Zahraa.. Twahira.. swiddiqa.. Zakiyya.. Radhiyya.. Mardhiyya.. Mubaraka.. Muhadditha. Kuinukia kwake: Nana Fatma aliinukia katika nyumba ya utumi, katika malezi ya babake mtumi wa mwenyezi mungu na mamake nana Khadija, akainukia kwa adabu za wazazi wake watukufu na yeye akawa ni mfano na kiigizo katika tabia mzuri, na alikua afanana zaidi sana na babake kitabia na maumbile, alikua mwekundu na nyele zake nyeusi na uso wake ulkua wafanana sana na babake na alikua akiingia kwa babake babake humuinukia akamkalisha karibu na yeye, na maneno yake pia yalikua yakifanana na ya mtumi. Kuolewa kwake: Uliolewa na Ali bin Abitwalib khalifa wa nne, na mahari yake yalikua ya sahali sana, nguo na mtandio na nguo nyengine na ayna ya nguo nyengine isokua na mikono ya kuvaa juu na kitanda chenye fremu ya majani ya mtende, na magodoro mawili, moja la malifu na majani na lengine la sufi ya kondoo, mito minne na mkeka, na mawe ya kusagia nafaka na beseni la shaba la kufulia, kiriba na kibunju cha mbao, chombo cha udongo na jagi la udongo, na busati la ngozi, mtumi alipoona haya mahari aliwaombea mungu akisema " ewe mola wabaraki watu wa nyumba hii ambao vyombo vyao vingi ni vya udongo". Watoto wake: Hasan, Husein, Zainab, Ummu kulthum, na Muhsin aliekufa akiwa mdogo. Kufa kwake: Alikua ni mtu wa kwanza katika ahlu beyt wa mtumi kumfuatia mtumi kwa kifo, na alikua akimlazimu sana babake akiwa karibu nae sana mpaka alipokufa babake hakuwahi kucheka tena kwa huzni aliokuwa nayo mpaka nae akafa baada ya babake kwa mda wa miezi sita akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, na katika kauli yenye nguvu ni kuwa alikufa Ramadhan mwaka wa kumi na moja hijriya, na Imam Ali mume wake ndie alismama kumtayarisha kwa kumuosha mpaka kumzika yeye mwenyewe, alizikwa katika maziara ya baqii. Amani iwe juu yako ewe Fatma Zahraa, mungu awe radhi nae na amridhishe, rehma na amani zimfikie bwana wetu mtumi Muhammad.