Maana ya ndoa na nguzo zake

 BISMILLAAH


MAANA YA NDOA NA NGUZO ZAKE


 Maana ya ndoa na nguzo zake:


 Maana ya ndoa (nikaah): ni agreement ambayo inapelekea kufaa kuundama kwa kutumika neno nikaah ama tazweej ama tafsiri ya maneno hayo katika lugha zengine.


 Nguzo za nikaah ni tano: 


1, Mume. 
2, Mke.
3, Walii. 
4, Mashahidi wawili. 
5, Swigha, (kuozesha na kukubali kuozeshwa).


  Ina maana ndoa sio lazima ifungwe kwa lugha ya kiarabu. Lakini lazima iwe kwa neno kuoa (nakuoza, nakuozesha).


  Ina maana walii akisema nimekupa zawadi badala ya kusema nimekuoza, basi ndoa itakua haijaswihi.


  Kuoa kwa neno la zawadi (hiba) ni moja katika khususiyaat za Mtume s.a.w, ama kwetu sisi haifai.


 Pengine mtu atauliza, mbona mume na mke wamehisabiwa kama nguzo mbili tafauti, na mbona mashahidi wasihisabiwe hivyo, tuseme shahidi wakwanza na shahidi wapili ndio nguzo ziwe sita? 
 Jawabu: kwasababu kuna masharti khaswa yanatakikana kupatikana kwa mume na hayapo kwa mke, na masharti khaswa yapatikane kwa mke na hayapo kwa mume, ama kwa mashahidi hamna tafauti katika masharti ya kupatikana kati yao wawili, ndio wakahisabiwa kama kitu kimoja.

 

 Wallaahu a'lam.