MAMBO HARAMU-HAJJ NA UMRAH

Mambo ambayo ni haramu kwa alie ingia kwenye ibada ya Hajj na Umrah kuyafanya, nayo ni mambo kumi:
1- kuvaa nguo ya mzunguko kwa mwanamume , kama kanzu na tshirt na viatu kama boot.
2- kufinikakichwa hata kama ni sehemu ndogo, kwa mwanamume.
3- kufinika uso kwa mwanamke na pia kuvaa gloves.
4- kutumia manukato (perfumes), ama kujifukiza kwenye mwili ama nguo na kila mahali anapoketi.
5- kutia mafuta ya nyele, kichwani na kwenye ndevu.
6- kufanya kitendo cha jimai ama vitangulizi vyake.
7- kukata nyele za sehemu yoyote katika mwili na kucha.
8- na kuwinda wanya wa bara.
9- kukata mimie ya haram, ispokua kama ni mti watumika kwa dawa na ahitaji hyo dawa, ama kama ni mti wa miba uko njiani.
10- kufunga nikaha, kwa mwenye kuoa na kuolewa kama wako kwenye ibada ya Hajj ama Umrah.

Lakini ibada ya Hajj na Umrah haziharibiki kwa kufanya haya mambo ya haramu ispokua kufanya kitendo cha jimai kabla ya kumaliza hizi ibada.