KUSMAMA ARAFAH-MAMBO YA WAJIBU NA SUNNAH

Na Jambo ambalo ni wajibu katika kusmama Arafah ni moja tu, nalo ni kuweko sehemu ya jabal la Arafah japokua kwa mda mchache tu siku ya tisa ya mfungo tatu, na wakati wake ni kwanzia baada ya adhuhuri mpaka kuzama kwa jua.

Na sunnah za Arafah ni nyingi na hizi ni baadhi yake :
- kuwa Arafah siku mzima mpaka lizame jua.
- kuleta tahlil ( لا إله إلا الله وحده لا شريك له له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير  )
- kuleta dhikri kwa wingi, takbir na talbiya ( labbeyka Allaahumma labbeyka. . . ) kusoma Qur'an, kumswalia mtumi, na dua nyingi zimepokea kutoka kwa Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) zapatikana kwenye vitabu vya hadithi.
- kuelekea qibla.
- kuwa na twahara kamili na kujisitiri.
- pia yasuniwa usmame kwenye jua kama si kali sana la kuumiza.
- kujumuisha swala ya adhuhuri na alasiri wakati wa adhuhuri, na kuchelewesha maghrib uswali na ishaa Muzdalifah.