KUSA'AYI SWAFAA NA MARWAH-MAMBO YA WAJIBU NA SUNNAH

Mambo ambayo ni wajibu katika kusaayi beina ya Swafaa na Marwah ni sita:
1- kuanza Swafaa amalizie Marwah.
2- Kusaayi iwe ni mara saba, kutoka Swafaa kufika Marwah ni mara moja, na kutoka Marwah kurudi swafa ni mara ya pili, atahisabu hivo mpaka atimize mara saba.
3- Ahakikishe ametimiza mwendo mpaka afike anapokwenda, lau atabakisha shubiri moja tu arudi itakua haijakamilika.
4- Kusaayi iwe kwenye njia iloelekana na jabal Swafaa ama Marwah, kwa maana hairuhusiwi uendee kuvulini kwako sana mpaka utoke kwenye njia ama kushotoni sana.
5- Asikatishe saayi kwa kufata mambo mengine, kama kumtafuta mtu alie potea, akikata saayi itabidi aanze tena mwanzo.
6- Kusaayi iwe ni baada ya tawaf ilioswihi, yani baada ya tawaf ya Umrah kama afanya Umrah, ama baada ya tawaf ya qudumi kama afanya ibada ya Hajj, na kama alkua hana wakati wa kusaayi baada ya tawaful qudumi akaenda Arafah basi hafai akitoka Arafah aje afanye ibada ya kusaayi, bali itamlazimu afanye ibada ya kusaayi baada ya tawaf ya ifadhwah, na kama hakuwahi pia kusaayi baada ya tawaf ya ifadhwah itabidi asubiri mpaka baada ya tawaf ya wadaai.

Na sunnah za saayi ni nyingi na hizi ni baadhi yake:
- kutoka msikitini kwa mlango wa Swafaa
- Kupanda jabali ya Swafaa na Marwah  kwa mwanamume.
- Kutia nia ya kusaayi akiwa ameelekea qibla, aseme natia nia kusaayi beina ya Swafaa na Marwah saayi ya Hajj ama Umrah mara saba, na wanazuoni wengine wamesema ni wajibu kutia nia.
- Awe na twahara na amejisitiri
- Kufuatanisha, kwa maana akianza kusaayi asikatishe, pia afuatishe kusaayi baada ya tawaf hapo kwa hapo.
Kuna na dua nyingi zimepokea kutoka kwa Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) zapatikana kwenye vitabu vya hadithi.