TAWAF-MAMBO YA WAJIBU NA SUNNAH

Mambo ambayo ni wajibu katika tawaf, sawa sawa ikiwa ni tawaf ya faradhi kama tawaf ya Hajj na Umrah na nadhiri na nyenginezo, ama ya sunnah kama tawaf ya qudumi ama yoyote ya sunnah, nayo ni mambo kumi:
1- kuwa twahara ya ya udhu na janaba.
2 - kuwa na twahara ya nguo zake na mwili wake na mahali anapo fanya tawaf.
3 - kujisitiri tupu, na tupu ya mwanamume ni kwanzia kitovu mpaka kwenye magoti, na mwanamke ni mwili wake mzima ikiwemo na miguu, ispokua uso na viganja vya mkono.
4- kuanza tawaf na kumaliza nikwenye hajarul aswad,na lau mtu  ataanza mahali kwengine haitohisibika mpaka afike kwenye hajarul aswad ndio yahisabika tawaf ya kwanza.
5- kutia nia wakati aanza tawaf kwenye hajarul aswad, atasema natia nia tawaf ya ifadha, ama ya Hajj, ama ya sunnah, ama ya nadhiri, na kadhalika.
6- kupakana na hajarul aswad wakati akianza tawaf na akimaliza, kwa maana mwili wake upande wa kushoto uwe umeelekea hajarul aswad, hapa ndio atatia nia aanze tawaf na akimaliza iwe upande wake wa kushoto umeelekea hajarul aswad kama alivoanza
7- Upande wake wa kushoto ndio utakua umeelekea Kaabah wakati wa tawaf, kwa maana atakwenda kinyume cha mwendo wa saa (anti-clockwise).
8- Mwenye kufanya tawaf awe nje ya Kaabah, mwili wake na nguo zake na kila kitu ambacho kimefungamana na yeye, vile vile awe nje ya hijri Isamil (nusu ya duara ilio ubavuni mwa Kaabah) na msingi wa Kaabah, kwa maana mtu akifamya tawaf nguo zake zisiguse hivi vitu.
9- Tawaf iwe ndani ya msikiti.
10- Azunguke Kaabah mara saba akianza hajarul aswad na kumalizia hajarul aswad.
11- Asikatishe tawaf kwa kufata mambo mengine, kama kumtafuta mtu alie potea, akikata tawaf itabidi aanze tena mwanzo.

Sunnah za tawaf:
1- kutembea kwa kwa miguu kwa anae weza.
2- asivae viatu kama hakuna jua la kuchoma ama baridi.
3- kutembea pole pole na kwa utulivu.
4- asizungumze bila dharura.
5- kuwa karibu na Kaabah ikiwezekana.
6- kubusu hajarul aswad kama hakuna zahma za kuumizana.
7- kuelekea hajarul aswad akitaka kuanza tawaf na kulisalimia kwa mko wake kwa kuligusa akiweko karibu ama kwa kushiria akiweko mbali.
8- kusalimia ruknul yamani mara tatu kila ukipita (pembe ya Kaabah ya upande wa kusini)

Na Sunnah za tawaf ni nyingi hapa tumeeleza kwa ufupi, kuna na dua nyingi zimepokea kutoka kwa Mtumi (rehma na amani ziwe juu yake) zapatikana kwenye vitabu vya hadithi.