IFRAD-TAMATTU'U-QIRAAN

Na mtu akitia nia ya ihram aruhusika kufanya ibada ya Hajj peke yake (ifrad ), ama afanye ibada ya Umrah katika miezi ya Hajj kisha afanye ibada Hajj mwaka huo huo (tamttu'u ), ama aziambatanishe hizi ibada mbili (qiraan), na iliokua bora katika hizi njia tatu ni kufanya kila ibada peke yake(ifrad), kama mfano afanye ibada ya Umrah nje ya miezi ya Hajj, kisha afanye ibada ya Hajj peke yake katika siku zake, kisha ilikua bora baada yake ni (tamttu'u) kisha ndio (qiraan).

Na mwenye kufanya (tamttu'u ) ama (qiraan ) itamlazimu yeye achinje mnyama kwa aya inayo sema: { na mwenye kufanya ( tamttu'u )  kwa kufanya Umrah kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiyekuwa na uwezo, afunge siku tatu akiwa haram na siku saba mtakapo rudi kwenu; hizi ni siku kumi kaamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawako karibu na Msikiti wa haram.} 2:196

Na kama atakavo toa fidya ya kuchinja ama kufunga mwenye kufanya ( tamttu'u ) ama ( qiraan ) pia atatowa fidiya mtu alie wacha mambo ya wajibu katika ibada ya Hajj.