MIPAKA NA WAKATI WA HAJJ NA UMRAH

Ibada ya Hajj na Umrah ina mipaka na nyakati zake, nazo zimegawanyika sehemu mbili, mipaka ya sehemu na mahali na mipaka ya nyakati za kufanya ibada hizi, kwa maana ibadi hizi zina siku zake maalumu kama Hajj, na zina sehemu maalumu za kutia nia ya ihram.

Na mpaka wa wakati wa ibada ya Umrah ni mwaka mzima, waeza kutia nia wakati wowote na ukaenda kufanya ibada ya Umrah, na mipaka ya wakati ya ibada ya Hajj ni katika miezi yake, kwa maana mtu hawezi kutia nia ya kufanya ibada ya Hajj ela katika hii miezi yake, nayo ni Shawwal (mfungo mosi ) na Dhulqaadah(mfungo pili) na siku tisa za Dhulhijjah (mfungo tatu)

Ama mipaka ya sehemu za kuingia kwenye ibada ya Hajj na Umrah ni kila mtu na mpaka wake kama alivoelezea Mtumi katika hadithi, nayo ni kama inavofuatia:
Watu wa Yemen mpaka wao ni Yalamlam.
Na watu wa Najdi, Najdi ya Yemen na Hijaaz mpaka wao ni Qarnil manazil.
Na watu wa Iraq, Iran, Afghanistan, India, Pakistan, na nchi zilioko karibu na hizi, mpaka wao ni Dhati irqi.
Na watu wa Sham, Syria,Jordan, Falastin,Turkey, na Misri, Libya, Tunisia, Algeria, na nchi ziloko karibu, mpaka wao ni Juhfah.
Na watu wa Madinah na watu wenye kuingia Makkah kupitia kwa Madinah mpaka wao ni Dhul huleyfah.

Na hii mipaka kama ilovokua maarufu iliwekwa wakati wa safari za zamani za kusafiri kwa wanyama, ama kwa sasa safari za ndege basi mtu uzuri atie nia ya kuhirimia anapo ondoka tu kwao.