SUNNAH ZA HAJJ NA UMRAH

Mambo ya SUNNAH: ni mambo ambayo hapati dhambi asipoyafanya wala halizimika kutoa fidiya, na pindi atafanya haya ya sunnah basi thawabu zake ni kubwa.

Sunnah za Hajj:
Sunnah za Hajj ni nyingi, na hizi ni baadhi yake:
1- kukithirisha kuleta talbiya(labbeyka Allaahumma labbeyka....) kila mahali, na imesuniwa zaidi kuleta kwa sauti kubwa kwa wanaume sio kwa wanawake.
2- kutanguliza ibada ya Hajj kabla ya Umrah , kisha atatoka mji wa Makkah kama ataka kurudi kufanya ibada ya Umrah ndio atie nia tena arudi Makkah afanye ibada ya Umrah.
3- kutufu tawaf ya qudumi, nayo ni tawaf ya mtu akiingia mji wa Makkah.
4- Kuswali rakaa mbili za baada ya tawaf ya qudumi.
5- Wanaume wamesuniwa kuvaa nguo ya chini ya wazi kama kikoy, na nguo ya kujitanda juu, nyeupe.
6- Kulala Muzdalifah usiku wa kuamkia Arafah.

Sunnah za  Umrah ni kuvaa nguo kama za Hajj, kukithirisha kuleta talbiya (labbeyka Allaahumma labbeyka. . . . . ) na kuswali rakaa mbili za tawaf.