MAMBO YA WAJIBU KATIKA IBADA YA HAJJ NA UMRAH

Mambo ya WAJIBU: nayo ni mambo ambayo mtu aspotimiza ibada itatimia ispokua atapata madhambi akiacha bila ya udhuru wa kukubalika, na pia atalazimika atoe fidiya nayo ni kuchinja mnyama.

Mambo ya wajibu katika ibada ya Hajj ni saba:
1- Kutia nia ya ihram kwenye mipaka, na atavua nguo za mzunguko kabla ya kutia nia avae nguo zile za kujitanda za ihram, ya juu na ya chini, na yapendekeza nguo za ihram ziwe nyeupe, pia imesuniwa aswali rakaa mbili za sunnah.
2- Kulala Muzdalifah usiku wa idi japokua mda mchache baada ya nusu ya usiku.
3- Kurusha vijiwe saba siku ya idi, Minaa, na wakati mzuri ni baada ya alfajiri mpaka kuzama jua la siku ya idi, na imesuniwa akirusha mawe alete takbiri kwa kila kijiwe.
4- kurusha vijiwe siku tatu za baada ya idi, kila siku vijiwe saba, na wakati wake ni baada ya adhuhuri mpaka kuzima kwa jua.
5- Kulala Minaa siku tatu za baada ya idi.
6- Kujiepusha na mambo ambayo ni haramu kwa mtu alie tia nia ya ihram, na tutaaeleza baadae mambo yenyewe.
7- Kutufu tawaf ya wada'a, nayo ni tawaf wanao fanya iabada ya Hajj ama Umrah huwa wakitufu kama wataka kutoka mji wa Makkah.

Na mambo ya wajibu katika ibada ya Umrah ni mawili:
1- Kutia ni ya ihram.
2- Kujiepusha na mambo ambayo ni haramu kwa kwa mtu alietia nia ya ihram.