NGUZO ZA HAJJ NA UMRAH

NGUZO: nayo ni mambo ambayo ibada haitimii mpaka zitimie nguzo zote, wala hazilipiki fidya lau mtu ataacha moja wapo bali ni lazima atimize nguzo zote.

Nguzo za Hajj na Umrah ni sita:
1- Kutia niya ya ihram, atasema natia niya kufanya ibada ya hajj ama umrah, na ikiwa amfanyia ibadaya hajj mtu mwengine atasema natia nia kufanya ibada ya hajj kwa niaba ya mtu fulani, na nia ya hajj mtu aweza kutia kwanzia baada ya mwezi wa Ramadhani mpaka mfungo tatu, ya imesuniwa mtu akitaka kutia nia ya hajj aoge na ajisafishe kila kitu mwilini, pia yasuniwa asema labbeyka Llahuma labeyka..... mpaka mwisho.
2- Kusmama katika jabal la Arafah siku ya Arafah, nayo ni tarehe tisa ya mfungo tatu, japokuwa mda mfupi baada ya adhuhuri, kwa hadithi ya Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) alposema:"ibada ya hajj ni kusmama Arafah.”
3- Tawaf ya ifadhah, na wakati wake waanza ikifika nusu ya usiku wa idi, yani baada ya Arafah.
4- Kusaayi beina ya Swafaa na Marwah, nayo inakua baada ya tawaf ya ifadhah.
5- Kupunguza nyele ama kukata zote.
6- Kuzipangilia hizi nguzo kama zilivo tajwa, kwa maana aanze na kutia nia ya ihram, kisha ni kusmama Arafah, kisha kutufu tawaf ya ifadhah, kisha kusaayi beina ya Swafaa na Marwah, kisha ni kunyoa ama kupunguza nyele.

Na nguzo za Umrah ni hizi hizi za Hajj ispokua katika Umrah hakuna kusmama Jabal la Arafah, hivi ndivo alivo fanya Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) ibada ya Hajj na Umrah na akatwambia: “chukueni kwangu namna ya kufanya ibada zenu"