Wingi na uchache wa heidh

Bismillaah.


Darsa la tatu:


Wingi na uchache wa heidh:


  Wingi wa heidh ni siku kumi na tano, hata kama haikufuatana katika kutoka. Na aghlabu ya heidh hua ni siku sita ama saba, na ndio wengi hupata hizo.


 Ama uchache wa heidh ni mchana na usiku, yani masaa ishirini na nne, lisipungue hata jisaa moja, hata kama itachukua mda wa masiku. kwa mfano anaona damu masaa mawili kila siku kwa mda wa siku 12.


 Ina maana akiona jisaa kila siku kwa mda wa siku zote kumi na tano ambazo ndio wingi wa heidh basi hio sio heidh, kwasababu ukiyajumuisha yote yanakua ni masaa kumi n tano, inakua bado haijafika uchache wa heidh, kwahivyo hio inakua ni damu fisadi.


 Na kama ataona damu kwa mda wa jisaa kila siku kwa masiku 24 basi hio pia sio heidh, kwasababu imepita wingi wa heidh ambayo ni siku kumi na tano.
Hii mida ya wingi na uchache wa heidh imewekwa na wanazuoni baada ya kufuatilia kwa kina hizi ada za wanawake wa kila sehemu na sampuli tafauti tafauti.


 Ama kinyume cha heidh ni twahara, uchache wake ni siku kumi na tano, kwasababu wingi wa heidh ni siku kumi na tano, na mwezi ni siku thelathini. Ama wingi wa twahara basi hauna idadi, kwakua mtu aweza kupata heidh mara moja tu katika umri wake, ama asipate kamwe. Ama aghlabu ya twahara ni siku 23 ama 24.


kwahivyo tunafahamu kutokamana na yaliyotangulia kua:
1: Damu ije baada ya miaka tisa takriban.
2: Isipungue masaa ishirini na nne.
3: Isizidi siku kumi na tano.
4: Twahara kati ya heidh mbili isiwe chini ya siku kumi na tano.

 

 Wallaahu a'lam.