SHARUTI ZA KULAZIMU HAJJ NA UMRAH

Na sharti za kulazimu Hajj na Umrah ni mtu kuwa muislamu, muungwana, aliekalifishwa na sharia, na kuwa na uwezo.
Na Sharuti za mtu kuhisabika kuwa anuwezo ni:
Ya kwanza awe na matumizi ya safari, chakula chake yeye mwenyewe na matumizi ya kulipia kina kinachohitajika kulipiwa safarini, kwanzia kutoka mja wake mpaka kufika Makkah na kurudi.
Sharuti ya pili awe na usafiri ama nauli ya kumfikisha Makkah kama yuko mbali na Makkah, kama yuko mji karibu na Makkah na aweza kutembea sio lazima awe na usafiri, na pia ni sharuti nauli iwe si deni wala si matumizi ya chakula cha mtu anae msmamia yeye, kama mke wake na watoto wake na wazee kama hawafanyi tena kazi, wala isiwe ni matumizi ya kulipia mahitajio ya nyumbani mengine
Sharuti ya tatu, barabara anayo safiria iwe salama, sawa kama ni bara ama baharini.
Sharuti ya nne, awe atapata chakula barabarani kwa bei yake ya kawaida, yani isiwe ni ghali sana kupita kiasi.
Sharuti ya tano, ni mwanamke aweko na mahrimu yake ama mume wake, ama akiwa na wanaume ajnabii lakini kukawa na wanawake zaidi ya watatu ambao waaminika basi haina neno, ataruhusiwa kufatana nao.
Sharuti ya sita, awe aweza kusafiri, kama ni mtu hawezi kusafiri kwa ndege ama kwa bahari ama usafiri wowote kwa sababu ya kudhurika afya yake basi pia huwa hajatimiza sharuti za uwezo.
Sharuti ya saba ni kipofu mpaka apate mtu wa kumshika mkono, kama hajapata mtu wa kumshika mkono kumpeleka kufanya ibada ya hajj basi pia itakua hajatimiza sharuti za uwezo.
Na mtu yoyote asie weza kuhiji kwa kukosana baadhi ya sharuti za uwezo, kama kipofu aliekosa wa kumpeleka, ama mzee asieweza usafiri, mgonjwa wa maradhi ambayo hayatarajiwi kutulia, itamlazimu amuakilishe mtu amfanyie ibada ya hajj kwa mali yake mwenyewe akiweza.