UFARADHI WA HAJJ NA UMRAH

Hajj na Umrah ni faradhi kwa dalili ya Qur’an na hadithi, dalili ya Qur’an {….. Na Mwenyezi Mungu amewafaradhia watu kuhiji Makkah kwa mwenye uwezo wa kufika, na mwenye kukanusha amri hii basi hakika Mwenyezi Mungu hahitaji lolote kwa walimwengu.} 3:97. Na dalili ya ufaradhi wa Hajj na Umrah {Timizeni ibada ya Hajj na Umrah kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.} 2:196.  Na dalili ya Hadithi: "uislamu umesmama kwa mambo matano: kukubali kuwa hapana mola anaefaa kuabudiwa kwa haki ila Allaah na kwamba mtume Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) ni mjumbe wake, kuswali swala tano, kutoa Zaka, kufunga mwezi wa Ramadhan, na kufanya ibada ya Hajj kwa mwenye uwezo" na ibada hizi zilifaradhiwa mwaka wa sita hijriya.