IBADA ZA MTUMI RAMADHANI

MAMBO ALOKUA AKIYAFANYA BWANA MTUMI (S.A.W) KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

Kila jinsi ya swifa njema nizenye kumthubutukiya mwenuezimgu mwingi wa kurehemu na rehma na amani ziwe juu ya kipenzi chetu.Ama baada ya kumshukuru Allah na kumtakia rehma kipenzi chake bwana mtumi (S.A.W ) 

Katika baadhi ya mambo alokiyafanya mtumi rehma na amani ziwe juu yake na akahimiza watu wafanye ni:-

Mtumi (S.A.W)  alikua akisoma sana Quran na akasisitiza watu juu ya kuisoma Quran kwani ni ndani ya mwezi huu ndio iliyoshukishwa ndani yake Quran..

~Mtumi (S.A.W) alikua akifanya ibada za sunnah na akawaambia maswahaba zake wazidishe ibada za sunnah katika mwezi huu mtukufu wa ramadhan kwani yoyote atakae fanya ibada ya sunnah ujra wake ni sawa na kufanya ibada ya faradhi na atakae fanya ya faradhi ni kma aliyefanya ibada hio mara  sabiini katika miezi mengne.

Alikuwa mtumi rehma na amani ziwe juu yake akifungulisha na kufuturisha baadhi ya maswahaba zake, na akiwahimiza maswahaba zake wafuturishane kwani atakae mfungulisha au mkufuturisha mtu aliyefunga katika mwezi huu wa ramadhan atasamehewa dhambi zake na atapata ujra kma wa yule aliyemfuturisha.

Alikuwa mtumi rehma na amani ziwe juu yake alkuaswali swala ya taraweh msikitini mwanzo kisha baadae akawa aswali kwake nyumbani kwa kukhofia isifaradhiwe swala ya taraweh kwa ummah wake na pengine itakua ni uzito kwa wengi kutekeleza ibada hini, baada yake sydna Omar bin Khatab ndio akakusanya watu kuswali taraweh kwa jamaa nyuma ya imam mmoja wakiswali rakaa ishirini.

Alkua mkarimu akipenda kutoa siku zote, lakini Ramadhini alikua mkarimu zaidi.

Rasul (S.AW)  katika kumi la mwisho alikuwa akikaa mskitini (itikaff) akilala huko na kuswali tahajud..akasema katika kumi la mwisho  la mwezi mtukufu wa ramadhan ndio ndani yake kuna usiku wa cheo, usiku uliobora kuliko miezi elfu moja..katika siku alizozitaja ambazo usiku huo huenda kupatikana ndani yake ni tarehe 21,23,25,27,29.

InshaAllaah tujipindeni haswaa hili kumi la mwisho kuzidisha kufanya ibada na kuwa wapole zaidi kwa waislamu wenzetu asaa na sisi tupate daraja kubwa kubwa na thawabu walio andaliwa waja wema katika mwezi huu mtukufu.