FAIDA ZA KUFUNGA MWEZI WA RAMADHAN

FAIDA ZA KUFUNGA MWEZI WA RAMADHAN

Watu wengi hufunga mwezi wa ramadhan kama wajib lakini ni wachache wanaojua faida za afya zipatikanazo kwa ajili ya kufunga. Kufunga ni mazoezi mazuri ikiwa utafunga inavo takikaniwa. Katika baadhi ya faida zake ni:

1.Kusafisha mwili:
Vyakula vingi haswa vya tayari kama vile vya mikebe hutiwa aina ya kemikali kusaidia visiharibike kwa haraka. Kemikali hizi hubadilika na kuwa sumu ndani ya mwili na baadae sumu hiyo kuhifadhiwa ndani ya mafuta ya mwili. Wakati wa kufunga, mafuta haya hochomwa na sumu na kemikali hizi hutoka mwilini.

2.Kupumzisha mashini za mwili:
Wakati wa kufunga, maida ya chakula tumboni hupumzishwa, ijapo kuwa kazi huendelea mwilini lakini katika viwango vya chini. zoezi hili husaidia katika kusaga chakula kwa kiwango kinacho tosha, kuleta balance ya maji mwilini na mwili kupata nishati mzuri.

3.Kupoza maradhi:
Baadhi ya tafiti zaonesha kuwa kufunga husaida katika kuponya maradhi kama vile allergy na maradhi ya mishipa. Baadhi ya wataalamu pia wadai kuwa hupelekea kupoa kwa vidonda vya tumboni kama vile ulcer.

4.Hupunguza sukari mwilini:
Kufunga hupelekea sukari ndani ya mwili kuvunjika (breakdown) kwa haraka, ili mwili kupata nishati. Jambo hili hupunguza uzalishaji wa insulin na kufanya pancreas (sehemu ya kusambaza sukari mwilini kutoka kwenye damu) kupumzika. Na faidayake ni kuwa sukari hupunguwa mwilini.

5.Kupunguza uzito wa mwili:
Wakati wa kufunga, sukari huyayushwa mwilini ili kutoa nishati (energy). Sukari ikipungua hupelekea kuchomwa kwa mafuta yaliyomo mwilini ili kuendeleza nishati na hii hupelekea mtu kupunguza uzito na mwili. Hata hivyo, pamoja na kufunga ni lazima kupunguza utumiaji wa sukari na mafuta mingi kwenye chakula na kuongezamatunda na mboga.

6.shinikizo la damu (pressure)
Kufunga ni moja ya njia ya kupunguza shinikizo la damu pasi na kutumia madawa. Husaida kupunguza athari ya magonjwa ya atherosclerosis ambayo ni kuzibika kwa mishipa ya damu na chembe za mafuta. Wakati wa kufunga, mafuta haya huyayuka, mwili  hufanya kazi kwa kiwango cha chini kwenye mipaka inayotakiwa na hii hupunguza maradhi ya shinikizo la damu (high blood pressure)

7. kuongeza kinga ya mwili na afya:
Mtu anapo funga na kufuturu kwa kula chakula kizuri cha afya, huongeza afya yake, hupunguza sumu mwilini, hupunguza uzito na mafuta. Vitamins huenea kwa haraka mwilini.

8. kupunguza uraibu:
Kufunga hupunguza hamu yautumiaji wa madawa ya ulevi na uraibu kama vile sigara, bhangi na marungi.