VITA VYA BADR

بسم الله الرحمن الرحيم

Baada ya udhia wa makafiri kuzidi juu ya waislamu Makkah, Waislamu walipata amri ya kugura kuenda mji wa madinah, wakiacha mali yao Makkah, makafiri  wa Makkah wakayavamia mali ya waislamu na kuenda kuyafanyia biashara mji wa Sham.
Mwaka wa pili baada ya Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) kugura kutoka Makkah  kuenda Madinah aliskia kuwa kuna msafara wa ma Qureysh watoka Sham waelekea Makkah na huo msafara ulkua ndani yake kuna mali ya waislamu yale walio yawacha mji wa Makkah, mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) baada ya kuona waislamu wamepata nguvu kiasi na akajua kuwa huu msafara unao ongozwa na Abu Sufyan (kabla hajaslimu) hauna ulinzi wa kutosha wa kuweza kuwaziwiya waislamu lau watataka kuuvamia na kuchukua mali yao.

Akatoka Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) na jeshi la maswahaba wanao fikia mia tatu na kumi na tatu wakikusudia huu msafara wa ma Qureysh.
Abu Sufyan baadae alipata habari kuwa Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) na maswahaba zake wametoka Madinah kwa nia ya kuvamia huu msafara, hapo hapo akabadilisha njia na akatuma mtu Makkah kuwambia makafiri wa Makkah kuwa Muhammad na maswahaba zake waja kuvamia mali yenu kwa hivo watoke makafiri wa Makkah wakapambane na waislamu, wakatoka watu wanao pata idadi yao alfu moja, kufika njiani wakapata habari kuwa Abu Sufyan amebadilisha njia na waislamu hawakuufikia msafara wake na mali yamefika salama Makkah.
Makafiri walposkia hivo hawakurudi Makkah bali waliamua waende wakapambane na waislamu hivo hivo.
Wakati huo waislamu walkua wamefika sehemu inayo itwa Badr na wao pia wamejua kuwa ule msafara walokua wameenda kuuvamia na kuchukua mali yao umefika Makkah kwa salama.
Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) aliwashauri maswahaba zake kuhusu kupigana na makafiri walpojua kuwa makafiri wameazimiya kuja kupambana nao, maswahaba wote wakamuunga mkono mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) kupambana na makafiri ilhali ya uchache wa idadi yao huku wakiwa na imani kubwa kwa Mola wao kuwa atawanusuru, huku Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) akiwapa bishara ya ushindi na kuwaonesha sehemu mbali mbali katika uwanja wa badr na kuwambia hapa atakufa kafiri flani, na hapa atakufa flani, na hapa atakufa flani, vita kuisha kila alietajwa atakufa sehemu flani alipatikana pale pale, haya ni katika miujiza ya Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake )
Usiku wa kupambaukia tarehe kumi na saba ya mwezi mtukufu wa ramadhani Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) alikesha akiomba na kunyenyekea kwa Mola wake huku akisema: " ewe Mola! nitimizie ulicho niahidi, nipe ulicho niahidi, ewe Mola! Hakika ukikiangamiza kipote hichi cha waislamu hutoabudiwa tena ardhini " huku akiendelea kuomba na kunyenyekea mpaka shali lake likamuamgukia, sydna Abubakar akamuona katika hali hii akamsikitikia huku akimwambia: yatosha hivo ulivo omba hakika Mola wako atakutimizia alicho kuahidi.
Usiku huu kukanyesha mvua ikawa ni neema kwa waislamu na niqma na adhabu kwa makafiri.
Asbuhi ya tarehe kumi na saba ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwaka wa pili hijriya, Mtumi ( rehma na amani ziwe juu yake ) alipanga jeshi la waislamu, na vita kuanza kwa mapambano ya watu wawili wawili na baadae kwa jumla, Mwenyezi Mungu aliwanusuru waislamu katika vita vya badr kwa kuwaletea malaika waliokua wakiwapiga makafiri, asema katika sura ya Anfal aya ya 9-10:
{Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu Mlezi, nae akawajibu kuwa nitawasaidia kwa Malaika elfu wanao fuatana mfululizo ○ Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zitulie, Na hakika haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu,Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.}
Mwenyezi Mungu akamnusuru Mtumi na maswahaba zake ingawa walikua wachache kwa idadi na silaha.
Na vita vya badr vilukua ushindi mkubwa kwa waislamu kwani waliuliwa wakubwa wa makafiri wa Makkah kama vile AbuJahli na Umeyya bin Khalaf (aliekua akimtesa Bilal) na wengine wengi, na ilifkikia idadi ya walio kufa katika makafiri watu sabiini na wengine sabiini wakashikwa kama mateka, wengine wakakimbia huku wakiacha mali yao na ghanima nyingi kwa waislamu, baadae mtumi akabakia badr siku tatu huku akizika mashahidi walio tangulia mbele za haki, na idadi ya waislamu walio kufa ilkua ni kumi na nne katika mia na kumi na tatu.

Hakika vita vya badr vilikua muhimu sana katika uislamu na za kupambanua beyna haki na batwil, na ilkua ndio mwanzo wa uislamu kupata nguvu na kuinuka jina lake.