MAZOEZI WAKATI WA RAMADHANI

MAZOEZI WAKATI WA RAMADHANI

Watu wengi huongeza uzito wa mwili wakati wa ramadhan kwa sababu hulala muda kidogo tu baada ya kula. Hii husababisha miili yao kupunguza kazi zamwili. Hata hivo, Ramadhan haifai kuwa ni wakati wa kulala tu bali mtu atakiwa afanye na mazoezi pia japo kidogo. Mazoezi husaida kwa kupunguza uzito, kubadilisha tabia mbaya kama vile uvivu, kuzidisha afya mwilini na kuusafisha mwili.

Kwa atakae kufanya mazoezi mwezi huu mwanzo aanze kwa mazoezi kidogo yasiotumia nguvu nyingi. Unapofunga, nguvu na nishati hupungua kwahiyo ni muhimu kupunguza kasi ya mazoezi.

Ni muhimu upunguze mazoezi yako kwa 50% wakati wa kufunga, muhimu zaidi nikuwa na uthabiti wa kuendelea zaidi ya kuwa na kiwango cha juu cha mazoezi. Kwa mfano, ni bora zaidi lau utafanya mazoezi ya chini kama kukimbia kwa nusu saa kama kufanya mazoezi ya dharubu kwa dakika kumi.

Mazoezi kama kuogelea, kukimbia ni bora zaidi wakati huu kuliko mengine ya dharubu kwa kuchunga nguvu za mwili pamoja na kutokwa na jasho mwilini itakayo sababisha upungufu wa mai.

Ni bora zaidi kufanya mazoezi baada ya kufuturu kuliko wakati wa swaum. Hii hupelekea misuli kujengeka na mafuta kuyayuka mwilini. Lazima kuwe na ratiba ya mazoezi na sio kufanya mazoezi wakati wowote.

La mwisho na muhimu zaidi ni kuuskiza mwili wako na kutojilazimisha kwa mazoezi uchokapo. Utakaposkia kisunzi ama kichwa kuumwa ni bora kupumzika na kuendelea baadae.