FALSAFA YA SWAUM

بسم الله الحمن الرحيم

Kila jinsi ya sifa njema astahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote, swala na salamu zimfikie kipenzi chetu Mtumi Muhammad bwana wa viumbe wote.

Ramadhan ni mwezi wa tisa katika kalenda ya ya Kiislamu, Jina la Ramadhan limekua ni jina la mwezi wa tisa katika historia ya waarabu kabla ya kuaanza Uislamu, Neno  lenyewe asli ni la kiarabu na maana yake ni joto kali.
Kila siku wakati wa mwezi huu, Waislamu duniani kote hutumia masaa ya mchana katika kufunga kamili. Kufunga ni moja ya nguzo za dini ya Kiislamu, na moja ya aina kubwa ya ibada kwa waisalmu. Kujiziwia kutokana na starehe za kila siku na kupambana na nia mbaya na tamaa hutukuliwa kama kitendo cha utwiifu kwa Allah, pamoja na kuwa ni kuisafisha nafs kutokana na dhambi na makosa.

Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislamu duniani kote hujiepusha na vyakula, vinywaji na mahitaji mengine ya kimwili wakati wa masaa ya mchana. Waislamu wanatakiwa kutumia mwezi huu kutathmini upya maisha yao katika muongozo wa Kiislamu. kuwasamehe wale walio tudhulumu, kuimarisha mahusiano na familia na marafiki, kujiepusha mbali na tabia mbaya - kwa nia ya kusafisha maisha yetu , mawazo yetu, na hisia zetu. Neno la Kiarabu (Swaum) "kufunga" linamaanisha "kujiepusha" - na maana yake si kujizuia tu na vyakula na vinywaji, lakini kuepukana na matendo mabaya, mawazo machafu na maneno ya upuuzi.

Wakati wa Ramadhani, kila sehemu ya mwili lazima ijizuiye na mambo maovu. Mdomo lazima ujiziwie kusengenya, macho yasitizame mambo yalo kinyume na sheria, mkono usiguse ama kuchukua kitu chochote ambacho si halali kwake, masikio ni lazima kuacha kusikiliza maovu na machafu, miguu ni lazima kuacha kwenda maeneo ya dhambi. Kwa namna hii, kila kiungo mwilini huwa kikifunga.
Kwa hiyo, kufunga sio kimwili tu, lakini ni kujitahidi kwa mwili wa mtu na nafsi na roho yake kwa kuepukana na maaswiya. Ramadhan ni wakati wa kuzidisha kumcha Mungu, kusafisha mwili na roho kutokana na uchafu na kuJIshughulisha zaidi na ibada.

Falsafa ya kufunga:
1- Kuimarisha imani na mapenzi
Imam Ali bin abi Twalib amesema kuwa "Hakika, mambo bora kufanywa na wacha Mungu ni kuamini Allah na mitumi yake, jihad inayoipa uislamu fakhri, kuwa mcha Mungu kwa namna inayotakiwa, kuswali na kutoa zaka na kufunga ambayo huepusha na adhabu. Ni juu yenu kufunga katika Ramadhan kwani ni kama ngao inaozuiya kutokana na Jahannam."

2- Kujenga Nafsi:
Kuijenga nafsi na kufanya subra katika ibada lazima ianze kutokana na kufunga.
Kuhusu hilo, Imam Ali bin Abi Twalib anasema "Kuepuka kumuasi Mungu yapelekea waumini kusalimika kutokamana na dhambi na huzinyosha nyoyo zao kwa Mungu, hivyo ni kusmama usiku kwa ibada na kufunga wakati wa siku za joto kali kwa hiyo wao hupata faraja Akhera baada ya kufanya bidii kufanya ibada dunia.

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'an Tukufu: "Hakika, kila dhiki imefuatana  na faraja". Hivyo kila kiu hufuatiwa na kuujenga moyo na kila njaa hufuatiwa na kupata faida.
Hakika kufunga ni tiba kwa magonjwa mengi ya kinafsi, siri kuu ya kufunga katika Uislamu ni kufikia afya ya nafsi, kwani magonjwa ya nafsi kama kibri na hasad na kujiona na menginio ndio magonjwa hatari sana kwa muislamu kuliko magonjwa mengine yanapatikana katika mwili.

3- Mapambano dhidi ya kiburi:
Mkubwa wa kiburi ni Shetani. Kwa hiyo, ili kupigana na kiburi tunapaswa kupigana na Shetani na kushiriki katika Jihad kubwa. Mapigano haya hayana mwisho, amani haitokei ndani yake na inaendelea mpaka Siku ya Qiyamah.

Moja ya malengo ya ujumbe wa manabii 'imekuwa mapigano dhidi ya kiburi."
Moja ya malengo makuu ya ibada kama vile kufunga ni kushinda kiburi. Kama Mungu angempa sifa ya kibri mmoja katika waja wake, basi neemah hiyo angewapa manabii wake. Lakini Mungu hapendi kiburi na akapendelea unyenyekevu kwao wao. Kwahiyo mitume wakawa ni wanyenyekevu mbele ya wacha mungu na mbele ya wengine japo wao ndio walokua wakiteswa. Mungu akawaonda imani yao kwa njaa, misukosuko na akawapa mitihani kupitia khofu na maradhi ili kuikuza imani yao.