Wakati wa heidh

Bismillaah.


Darsa la pili:


Wakati wa heidh :


 Heidh inayo wakati wa kuanza, na ina wingi na uchache. Ama kinyume chake abayo ni twahara basi ina uchache na wala haina wingi.


 Tukianza na wakati wa heidh: heidh inaanza anapofika bint wa hawaa miaka tisa kwa hesabu ya mwezi, yani kwa miaka ya hijriya, na katika somo hili daima hesabu zitatumika za kimwezi sio za kijua, kwahivyo  tukisema mwezi tunakusudia siku thalathini.


Na haidhuru kupungua kwa chini ya siku kumi na sita, yani akiona damu kabla atimie miaka tisa kwa siku kumi basi damu hio ni heidh. Ama akiona damu kabla ya miaka tisa kwa siku ishirini na zaidi.. kama mwezi na mwaka na kadhalika, basi damu hio itakua si heidh.


 Ikiwa ataona damu na ikawa baadhi ya masiku ni kabla ya wakti wa heidh na masiku mengine ni ndani ya wakti wa heidh, basi aloiona ndani ya wakati ndio heidh. kwa mfano, kama amepata heidh kabla ya kuingia miaka tisa kwa siku ishirini, kisha ikaendelea mpaka kabla ya miaka tisa kwa siku kumi, basi heidh ni kutoka kabla ya miaka tisa kwa siku kumi na sita, ama siku nne zilotangulia sio heidh.


 Pengine mtu atauliza, damu inayotoka kabla ya miaka tisa kama sio heidh ni damu gani? 
 Jawabu: ni damu fisadi, ambayo tutaiashiria kwa urefu ikifika wakti wake inshaallaah.


 Na mwanamke anapopata heidh ndio hua ashabalighi, huwajibika kufanya takalif za sheria kama swala na funga na mengineo.

Wallaahu a3lam