SWAUM ZA SUNNAH

SWAUM ZA SUNNAH:

Ni sunnah  kufunga juma tatu na alkhamisi katika kila wiki.

Kufunga siku tatu kila mwezi wa kiislamu  na zikiwa ni siku tatu za mwezi  kukamilika ni bora zaidi  (13, 14, 15) maana atakua amepata sunnah mbili kwa wakati mmoja.

Kufunga siku sita za mwezi wa shawwal, nao ni mwezi baada ya ramadhani, na hizi siku huanza baada ya siku ya idi, wala si lazima kufunga hizo siku sita kwa kufatisha.

Kufunga siku ya arafa, nayo ni tarehe tisa ya mwezi wa dhulhijja(mfungo tatu), vile vile ni suunah kufunga siku nane kabla ya siku ya arafa.

Kufunga tarehe tisa na na kumi ya muharram (mfungo nne)